Neymar.
Mshambuliaji nyota wa
Brazil Neymar amefafanua kuwa kelele za mashabiki ambao wanamzomea
wakati wa mchezo wa robo fainali ya michuano ya Olimpiki dhidi ya timu
ya Honduras hazikuwa zikimsumbua. Brazil
ambayo ilishinda mchezo huo kwa mabao 3-2 ulikuwa na ushindani wa hali
ya juu na kupelekea Honduras kupewa kadi nane za njano na mbili nyekundu
kutokana na rafu walizokuwa wakicheza ili
kuwazuia vijana wa Brazil. Neymar anayekipiga katika klabu ya Santos ambaye alikuwa akizomewa kufuatia kusababisha Wilmer Crisanto kupewa kadi nyekundu kwa kumkwatua, amesisitiza kuwa mashabiki waliokuwa wakimzomea walimuongezea nguvu ya kufanya bidii zaidi. Mashabiki hao walikuwa wakimzomea mchezaji huyo kwamba anapenda kujiangusha lakini mwenyewe alijitetea kuwa haikuwa tabia yake kwani wakati anaanguka lazima kuna anakuwa amemchezea vibaya. Brazil itasafiri kuelekea jijini Manchester wakati watakapokwaana na Korea Kuisni katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo utakaochezwa Jumanne.

No comments:
Post a Comment