Tetesi za J'nne magazeti ya Ulaya


DAVID SILVA KUONDOKA MAN CITY, LIVERPOOL HAIMTAKI ANDY CARROLL

Manchester City inaweza kumpoteza kiungo wake nyota, David Silva, aliyezaliwa miaka 26 iliyopita, baada ya mazungumzo ya kuongeza mkataba naye kuvunjika.
Andy Carroll
Andy Carroll anatakiwa na West Ham na Newcastle 
Liverpool itamuambia Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23, aamue mustakabali wake hadi mwishoni mwa wiki hii, huku Wekundu hao wakifikiria kumuuza Tottenham, iliyoonyesha nia ya kumsajili.
Mchezaji anayetakiwa na Manchester City, Daniele De Rossi, mwenye umri wa miaka 29, anajianda kukataa ofa ya klabu hiyo ya Ligi Kuu England, abaki Roma.
West Ham inajipanga kujaribu bahati yake kwa kiungo Matt Jarvis, mwenye umri wa miaka 26, huku wakiwa karibu kumnasa winga mwenye umri wa miaka 25 wa Rennes, Razak Boukari.
Queens Park Rangers inataka kumsajili beki wa Tottenham, Michael Dawson, mwenye umri wa miaka 28.
Habari kamili: The Times  (subscription required)
Tottenham haina nia ya kumsajili m shambuliaji wa Arsena, Marouane Chamakh mwenye umri wa miaka 28.
Tottenham inataka kumfuata kiungo wa Roma, Miralem Pjanic, mwenye umri wa miaka 22, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Sunderland haitapigwa bao katika mshahara au ada ya uhamisho na klabu nyingine zinazomuwania pia, kiungo wa Manchester City, Adam Johnson, aliyezaliwa miaka 25 iliyopita.
Roberto Martinez
Kocha wa Wigan, Roberto Martinez alikuwa anatakiwa na Liverpool
Kipa wa Blackburn, Mark Bunn, mwenye umri wa miaka 27, anatakiwa na klabu ya Norwich City.
Wolves imewaambia wachezaji wanaotaka kuondoka, Steven Fletcher na Matt Jarvis kuzingatia mikataba yao na kubaki Molineux.

MARTINEZ AFICHUA KUHUSU LIVERPOOL

Roberto Martinez amesema alikataa kazi ya kuikochi Liverpool.
Eden Hazard, aliyezaliwa miaka 21 iliyopita, anaamini hatasumbuliwa na kupigwa 'ngwala za nguvu' na mabeki wa Ligi Kuu, baada ya kuuanza vizuri msimu akiwa na Chelsea.
Habari kamili: The Times  (subscription required)

BALOTELLI SASA APOKONYA LENZI ZA WAPIGA PICHA

Mario Balotelli amegundua njia mpya ya kuwazuia wapiga picha kumpiga picha, anawachukulia lenzi zao.