Boris Bunjak.
Timu ya Azam imempa
mkataba wa miaka miwili kocha mpya Boris Bunjak kutoka Serbia ambaye
atarithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Stewart Hall kutoka
Uingereza. Stewart
alitimuliwa kibarua cha kuinoa klabu hiyo Jumatano iliyopita kufuatia
kikao cha bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo baada ya kukiuka masharti
aliyopewa na bodi hiyo ya kutompanga mchezaji Mrisho Ngassa katika
mchezo wa fainali
ya michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika hivi
karibuni. Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo asubuhi Makamu Mwenyekiti wa Azam,
Said Mohamed amesema kuwa baada ya bodi pamoja na menejimenti wa klabu
hiyo kupitia wasifu wa makocha ambao walikuwa wametuma maombi ya kuinoa
klabu hiyo waliridhishwa na wasifu wa Bunjak. Mohamed
aliendelea kusema kuwa Bunjak mwenye umri wa miaka 54 ambaye ana cheti
cha ukocha kinachotambulika na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA amewahi
kufundisha vilabu 15 tofauti barani Asia na Ulaya na hii ni mara ya
kwanza kufundisha Afrika. Akihojiwa
mara baada ya utambulisho huo Bunjak amesema kuwa amefurahi kuteuliwa
kuifundisha klabu hiyo kwasababu ni klabu yenye uchu wa mafanikio na
kutwaa mataji mengi zaidi. Mohamed
amesema kuwa kocha Vivek Nagul kutoka India ambaye alikuwa anakaimu
nafasi ya Stewart ataendelea kuwa kocha wa vijana wakati msaidizi wa
Bunjak atabakia kuwa Kalimangonga Ongala.
No comments:
Post a Comment