Kirani James wa pili kutoka kulia akimaliza mbio za mita 400.
Janailikuwa ni siku ya
furaha kwa kisiwa cha Grenada kilichopo Caribbean baada ya mwanariadha
Kirani James kunyakuwa medali ya dhahabu katika mbio za mita 400 kwenye
michuano ya olimpiki jijini London. Wananchi
wa Grenada walikuwa akicheza, kushangilia na kupeperusha bendera katika
mitaa ya nchi hiyo
wakati James mwenye umri wa miaka 19 aliposhinda
medali ya kwanza ya dhahabu kwa nchi hiyo akitumia muda wa sekunde
43.94. Waziri Mkuu
wa nchi hiyo Tillman Thomas alitangaza siku ya Jumanne kuwa ya
mapumziko kiserikali huku akimwelezea mwanariadha huyo kama mfano wa
kuigwa na vijana wengine wan chi hiyo. Thomas
alimsihi James kuendelea kufanya vizuri zaidi katika michuano mingine
ili kuliwakiisha vyema taifa hilo na kuendelea kudumisha nidhamu ili
aweze kufanikiwa. Watu
wa Grenada wanategemea ushindi wa James utakuza jina la taifa hilo
ambalo lina idadi ya watu zaidi ya 100,000 na uchumi mkubwa ukitegemea
sekta ya utalii.
No comments:
Post a Comment