Anikulapo Kuti akiwa na wake zake watatu wakati wa ndoa yao.
Fela Anikulapo Kuti, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
ametoa mpya kwa walimwengu kwa kufunga ndoa na wanawake watatu.
Mtu huyo ambaye anatumia jina la mwanamuziki aliyevuma zamani wa Nigeria, hayati Fela Anikulapo Kuti, amefunga ndoa hiyo kufuatia mchungaji wa kanisa lake nchini humo kuwaambia waumini wake kwamba
Mtu huyo ambaye anatumia jina la mwanamuziki aliyevuma zamani wa Nigeria, hayati Fela Anikulapo Kuti, amefunga ndoa hiyo kufuatia mchungaji wa kanisa lake nchini humo kuwaambia waumini wake kwamba
wanaweza kuoa
wanawake wengi, jambo ambalo limeleta mkanganyiko mkubwa kwa waumini wa
madhehebu ya Kikristo barani Afrika.
Ndoa hiyo ilifungwa kama
kawaida, ambapo watu hao wanne waliapa kuwa mume na wake zake,
wakishuhudiwa na watu kibao huku kiongozi aliyeifungisha ndoa hiyo
akinukuu vifungu vya Biblia ambavyo hutumiwa na Wakristo wote.
Tukio
hili limeleta mkanganyiko mkubwa na kuwaacha watu wengi wakijiuliza
mengi kuhusu madhehebu ya Kikristo yanavyojiingiza katika matendo
yasiyoendana na imani yao, ambayo inasisitiza mke au mume kuwa na mwenza
mmoja tu.
No comments:
Post a Comment