Mwanariadha nyota wa mbio
ndefu kutoka Uingereza Mo Farah amefanikiwa kunyakuwa medali ya dhahabu
katika katika mbio za mita 10,000 kweye michuano ya Olimpiki
inayoendelea jijini London na kukamilisha usiku wenye mafanikio zaidi
kwa wanamichezo wa Uingereza wanaoshiriki michuano hiyo. Katika
muda huohuo ambao Farah alinyakuwa medali hiyo, wanamichezo wengine
wawili nao walishinda
medali za dhahabu ambao ni Jessica Ennis alishinda
mashindano ya kurusha mkuki huku Greg Rutherford naye akiibuka kidedea
katika mashindano kuruka chini. Farah
mwenye umri wa miaka 29 ambaye pia ni bingwa wa dunia wa mbio za mita
5000 alimaliza mbio hizo akitumia muda wa dakika 27 na sekunde 30.42
huku Galen Rupp ambaye wanafanya mazoezi pamoja akinyakuwa medali ya
fedha kwa kukamata nafasi ya pili wakati nafasi ya tatu ikishikiliwa na
Tariku Bakele. Ushindi
huo wa Farah umekomesha ufalme wa wanariadha wa Ethiopia ambao wamekuwa
mabingwa wa mbio za umbali kwenye michuano hiyo mara nne huku
akimsimamisha mwanariadha nyota kutoka huko Kenenisa Bakele kushinda
michuano hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.
No comments:
Post a Comment