Usain Bolt akiwa na Yohane Blake kushoto na Warren Weir.
Mwanariadha nyota wa mbio
fupi Usain Bolt kutoka Jamaica amejinasibu kuwa ndiye mwanariadha pekee
wa kihistoria kuwepo baada ya kufanikiwa kutetea medali zake katika
michuano ya olimpiki jijini London. Bolt
alitamba hivyo baada ya kufanikiwa na kuwa mwanariadha wa kwanza
kutetea ubingwa wake katika mbio za mita 100 na 200 katika michuano ya
olimpiki. Kabla ya
fainali ya mbio hizo za mita 200 Bolt alidai
kwamba anaweza kuvunja
rekodi yake ya dunia aliyoweka ya muda wa sekunde 19.19 lakini baada ya
fainali hiyo alikiri kuwa alikuwa na kasi lakini hakuwa katika kiwango
chake cha kawaida na kuonya kuwa bado hajafikiria kustaafu kwani
anaupenda mchezo huo. Katika
mbio hizo Jamaica ndio walionekana kutamba kwa kunyakuwa medali zote
ambapo Yohane Blake alinyakuwa medali ya fedha kwa kushika nafasi ya
pili huku mwanariadha anayechipukia Warren Weir akipata medali ya Shaba
nyuma ya Bolt ambaye alitumia muda wa sekunde 19.32.
David Rudisha.
Kwa upande wa mbio za
mita 800 wanaume, mwanariadha nyota kutoka Kenya David Rudisha
alifanikiwa kuweka rekodi mpya katika mbio hizo akitumia muda wa dakika
moja na sekunde 40.91 na kuondoka na medli ya dhahabu. Rudisha
ambaye ana umri wa miaka 23 alivunja rekodi yake mwenyewe aliyoweka
katika michuano ya olimpiki iliyofanyika jijini Beijing mwaka 2008 na
kuwa mwanariadha wa kwanza katika mbio za umbali huo kufanya hivyo
kwenye historia ya michuano hiyo. Nafasi
ya pili katika mbio hizo ilichukuliwa na Nijel Amos kutoka Btswana
ambaye ana miaka 18 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mkenya mwingine
Timothy Kitum ambaye naye ana umri kama wa Amos.
No comments:
Post a Comment