Barack Obama.
Rais wa marekani Barack
Obama amekikpongeza kikosi cha timu ya taifa ya Marekani cha wanawake
kwa kufanikiwa kunyakuw medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki
jijini London kwa kuisambaratisha Japan kwa mabao 2-1 katika mchezo wa
fainali uliochezwa katika Uwanja wa Wembley jana. Obama
aliyasema hayo wakati alipotembelea kituo cha mazoezi cha olimpiki
nchini humo kilichopo Magharibi mwa jimbo la Colorado kwa kuipongeza
timu hiyo kwa kulipiza kisasi baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya
Kombe la Dunia dhidi ya Japan kwa changamoto ya mikwaju ya penati mwaka
jana. Nyota wa
mchezo huo alikuwa alikuwa Carli Lloyd ambaye alifunga mabao mawili
katika mchezo huo yaliyoiwezesha timu yao kunyakuwa dhahabu ikiwa ni
kama kifuta machozi baada ya mchezaji huyo kukosa mkwaju wa penati ambao
uliipa Japan Kombe la Dunia mwaka jana. Timu
ya soka ya wanawake ya Marekani imekuwa na mafanikio toka soka la
wanawake liongezwe katika michuano ya olimpiki wakiwa tayari wameshinda
michuano ya olimpiki ya mwaka 1996 iliyofanyika jijini Atlanta, Athens
mwaka 2004 na Beijing mwaka 2008. Obama
pia aliwapongeza wanamichezo wote ambao wameshiriki michuano ya
olimpiki na olimpiki kwa walemavu mwaka huu jijini London kwa heshima
kubwa waliloletea taifa hilo.
No comments:
Post a Comment