Wachezaji wa soka wa timu
ya taifa ya Korea Kusini wameongezewa motisha ya kutolitumikia jeshi la
nchi hiyo kama watafanikiwa kuwafunga wapinzani wao Japan na kunyakuwa
medali ya shaba katika michuano ya olimpiki. Hatua
hiyo ni ya kushangaza toka mshambuliaji wa kimataifa wa nchi hiyo
anayecheza klabu ya Arsenal Park Chu-Young kuachwa katika kikosi cha
timu hiyo katika mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia na
kulazimika kuomba msamaha kwa kuchelewa kujiunga na jeshi na kuchukua
uraia wa Monaco.
Akihojiwa
kuhusiana na suala hilo, Kocha wa timu hiyo Hong Myung-Bo alikiri kuwa
ni kweli kama wakipata medali ya shaba ya kushika nafasi ya tatu katika
michuano hiyo wachezaji watapata msamaha wa kwenda jeshini kitu ambacho
ni lazima kwa raia yoyote kwa Korea Kusini. Kocha
huyo aliendelea kusema kuwa suala hilo halina umuhimu sana kwani
madhumuni yao makubwa ni kuifunga Japan na kuwapa furaha mamilioni ya
mashabiki watakaokuwa wkiwatizama huko nyumbani. Japan
imewahi kutwaa medali ya shaba katika michuano ya olimpiki iliyofanyika
jijini Mexico City mwaka 1968 na wamepata nafasi hiyo tena dhidi ya
mahasimu wao Korea Kusini baadae leo mchezo ambao unatarajiwa kuwa mkali
na kusisimua.
No comments:
Post a Comment