Friday, August 10, 2012

AJALI MBAYA ENEO LA PWANI YAUA ZAIDI YA WANNE ASUBUHI HII.

Kamanda Mpinga.
Mzimu wa ajali za barabarani wazidi kulitesa Taifa baada ya ajali mbaya ya juzi huko mkoani Tabora iliyopelekea vifo vya watanzania 17 na wengine 78 kujeruhiwa ,watu wengine zaidi ya wanne wameripotiwa kufa na wengine zaidi ya 15 kujeruhiwa vibaya baada ya ajali mbaya kutokea eneo la Makole/Wami mkoani Pwani katika barabara kuu ya Chalinze - Tanga asubuhi ya leo.

Mwandishi wa mtandao huu wa funzblack.blogspot.com, anaripoti kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili na malori mawili kugongana .
Wakati katika ajali ya pili malori mawili yamegongana na kuziba njia huku wananchi eneo hilo la Lugoba wamejazana eneo la tukio kuiba mafuta katika lori hilo la mafuta ambalo limeanguka kutokana na ajali hiyo huku barabara ya eneo hilo ikiwa imefungwa hadi sasa .
Jitihada za kumtafuta kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Bw Mohamed Mpinga na kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani bado zinafanywa.

No comments: