Mbwana Samatta.
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), limesema linatarajia kuliandikia barua Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kuilalamikia klabu ya TP Mazembe ya DR Congo kuhusu kuwazuia wachezaji wake, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kujiunga na timu za taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah amesema kwa sasa wapo katika mchakato wa kuandika barua hiyo ili kuifahamisha Fifa iweze kuichukulia hatua klabu hiyo.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah amesema kwa sasa wapo katika mchakato wa kuandika barua hiyo ili kuifahamisha Fifa iweze kuichukulia hatua klabu hiyo.
“Tunatarajia kuandika barua ya malalamiko kwa Fifa kutokana na TP Mazembe kutowaruhusu wachezaji wetu, tupo katika mchakato, tunatarajia kuiwasilisha ndani ya wiki hii.
“Naamini iwapo tutaandika barua hiyo, itatusaidia kupata haki yetu ya msingi kwa wachezaji kuruhusiwa ndani ya muda muafaka pindi wanapohitajika,” alisema Osiah.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa sheria za Fifa, mchezaji anatakiwa atue katika timu ya taifa siku nne kabla ya mechi, ikiwa ni pamoja na klabu husika kupewa taarifa mapema, jambo ambalo lilifanyika lakini upande wa pili haukuonekana kujali.
No comments:
Post a Comment