Ye Shiwen.
Muogeleaji Ye Shiwen
kutoka China amevunja rekodi ya dunia ya mita 400 katika mchezo huo na
kunyakuwa medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki inayoendelea
jijini London, Uingereza. Shiwen
mwenye miaka 16 aliweka rekodi hiyo akitumia muda bora wa dakika
4:28:43 mbele ya bingwa wa dunia
kutoka Marekani Elizabeth Beisel na Li
Xuanxu ambaye pia anatoka China. Muogeleaji
huyo alivunja rekodi ya muda wa dakika 4:29:45 ambayo ilikuwa imewekwa
na Stephanie Rice kutoka Australia katika michuano ya olimpiki
iliyofanyika Beijing mwaka 2008. Muogeleaji
kutoka Uingereza Hannah Miley ambaye alishinda medali ya fedha katika
mashindano ya dunia mwaka jana na kutegemewa kufanya vizuri katika
mashindano hayo alishindwa kutamba baada ya kumaliza katika nafasi ya
tano. Mara baada
ya mashindano hayo Miley aliomba radhi mashabiki wake ambao walitarajia
atafanya vizuri ambapo kwasasa amesema anahamishia nguvu zake katika
mbio za kuogelea za mita 200 kuhakikisha anafanya vyema.
No comments:
Post a Comment