Roger Federer.
Wacheza tenisi nyota
Roger Federer na Serena Williams wameanza vyema kampeni zao za
kuhakikisha wanaondoka na medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki
baada ya kushinda michezo yao ya kwanza. Federer
kutoka Switzerland ambaye anashikilia namba moja katika orodha za ubora
za mchezo huo
duniani kwa upande wa wanaume alifanikiwa kumfunga
Alejandro Falla kutoka Colombia kwa 6-3 5-7 6-3. Kwa
upande wa wanawake Williams ambaye anashika nafasi ya nne katika orodha
za ubora alifanikiwa kumfunga kirahisi Jelena Jankovic kutoka Serbia
kwa 6-3 6-1 na kufanikiwa kutinga raundi ya pili. Kim
Clijsters kutoka Ubelgiji ambaye amepanga kustaafu mchezo huo mwishoni
mwa mwaka huu alifanikiwa kumfunga Roberta Vinci kutoka Italia kwa 6-1
6-4 ambapo sasa anatarajiwa kukutana na Carla Suarez wa Hispania katika
mzunguko wa pili wakati Serena atakutana na Urszula Radwanska wa Poland.
Federer atacheza na Julien Benneteau kutoka Ufaransa ambaye alimfunga kwa seti tano katika michuano ya Wembledon iliyopita.
No comments:
Post a Comment