Sunday, July 29, 2012

SPURS YAKUBALI KUMUUZA MODRIC KWA PAUNDI MILIONI 36.

 
 Luka Modric.
Klabu ya Tottenham Hotspurs imekubali kumuuza kiungo wake Luka Modric kwa ada ya paundi milioni 36 kwenda klabu ya Real Madrid ya Hispania. Kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia tayari alishasema kuwa atajiunga na Madrid lakini alikuwa akisubiria klabu hizo kufikia makubaliano. Modric kidogo apoteze
nafasi yake ya kwenda Madrid baada ya kukataa kusafiri na Spurs katika ziara huko nchini Marekani lakini viongozi wa Madrid walimlazimisha kuomba msamaha na kwenda kwenye ziara hiyo. Mkataba huo utamaliza utata wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye alianza kushinikiza kuondoka kwenda Chelsea mwaka uliopita lakini alikataliwa na klabu yake hiyo.

No comments: