Mashabiki wa Simba leo
wamemtembezea kichapo mama mmoja aliyekuwa amevalia jezi ya timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars yenye nembo ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), kosa
lake likiwa kukaa kwenye jukwaa walilokuwa wamekaa wao. Haikuweza kufahamika mara
moja, mashabiki wa Simba wana bifu na TFF au hawapendi timu ya
Taifa.
Mama
huyo alikimbizwa huku akipewa kichapo hadi kutokwa damu, kabla ya kuokolewa na
Polisi waliomteremsha jukwaani. Aliporwa vitu vyake kama pochi na kadhalika.
Baadaye akiwa amekwishaokolewa na askari, ndipo msamaria mwema mmoja, albino,
akamuokotea baadhi ya vitu na kuwakabidhi askari. Huwezi kulipa jina lingine
tukio lile, zaidi ya udhalilishaji wa kijinsia. Alikuwa anatia huruma mama huyo
wakati anahangaika kujitoa kwenye kundi la mashabiki wa kiume wa Simba,
iliyofungwa 3-1 na Azam leo katika Robo Fainali ya Kombe la Kagame
No comments:
Post a Comment