William Mhando.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanesco William Mhando.Wakati Wizara ya Nishati na Madini ikitarajiwa kuwasilisha bajeti yake kwa mwaka wa Fedha 2012/2013, mvutano miongoni mwa wabunge umezidi kutanuka kiasi cha kuhatarisha mjadala wa bajeti ya wizara hiyo.
Lakini wakati hali hiyo ya mvutano ikibainika miongoni mwa wabunge, kile kinachoelezwa kuwa ni mvutano kati ya viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa upande mmoja na viongozi wa TANESCO waliosimamishwa umechukuwa sura mpya, ikielezwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO (aliyesimamishwa), William Mhando, ana maslahi katika zabuni ya kusambaza vifaa vya ofisi ya kampuni ya mkewe, Eva Mhando inayoitwa Santa Clara Supplies Co. Ltd.
Kampuni hiyo ya Santa Clara Supplies Limited inadaiwa kupewa mkataba wa Sh.884,550,000 na TANESCO kwa ajili ya kusambaza vifaa hivyo.
Lakini akizungumza ofisini kwa Raia Mweam jana Jumanne, Mhando alikiri kuitambua kampuni hiyo si mali ya familia yake bali mkewe, Eva ambaye awali alikuwa akifanya kazi TANESCO ndiye ameajiriwa na kampuni hiyo.
KAMPUNI KUPEWA ZABUNI:
Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa Mhando, akiwa Mkurugenzi wa TANESCO, bila kujali mgingano wa kimaslahi aliacha mchakato wa kuipa zabuni kampuni hiyo uendelee na hatimaye kampuni hiyo ikashinda zabuni hiyo ya kusambaza vifaa vya ofisi kwa TANESCO.
Mhando anadaiwa kuipa kampuni hiyo iliyosajiliwa April 04, 2011, taarifa zaidi zikieleza kuwa, kampuni hiyo ilianza na mataji wa Sh. Miliomi kumi na wanahisa wake ni Fred Willliam, Veronica William na Steven William na kwa mujibu wa usajili wa kampuni hiyo, wanahisa hao pia ni makaimu wakurugenzi.
Maelezo ya usajili wa kampuni hiyo ya Santa Clara Supplies Co. Ltd, ambayo Raia Mwema imefanikiwa kuyaona, yanaonyesha kuwa ipo katika kitalu namba 204, Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.
Kwenye orodha ya wanahisa na makaimu wakurugenzi wa kampuni hiyo majina ya Fred na Veronica, yamebainika kuwa ni watoto wa Mhando.
MAJIBU YA MHANDO.
Katika kufafanua kuhusu suala hilo, Mhando alisema wakati akiwa TANESCO katika ngazi za chini alikuwa akifanya kazi katika shirika hiloo na mkewe, Eva.
Hata hivyo kwa mujibu wa maelezo yake, mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo pekee la kusambaza umeme nchini, Wizara ya Nishati na Madini, ilimwandikia barua ya kutaka mkewe aachishwe kazi ili kuepusha uwezekano wa kuwapo kwa mgongano wa kimaslahi.
“Mke wangu aliacha kazi, lakini tulikuwa na kampuni hiyo ya stationery Kariakoo na kwa sababu biashara haikuwa nzuri kutokana na uwezo mdogo wa kifedha, tuliuza kampuni hiyo mwaka jana.
Mke wangu aliajiriwa tu katika kampuni hiyo baada ya kununuliwa ili waweze kutumia uzoefu wake katika kuiendesha.
“Sasa kwa nafasi ya mke wangu, yeye ni Mtendaji wa hiyo kampuni lakini shughuli zote za kutafuta shughuli zote za kutafuta zabuni zinafanywa na wakurugenzi wa kampuni hiyo, si mke wangu.
“Kwahiyo, walipoomba kazi TANESCO hatua zote zilifanyika kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sharia na kampuni hiyo ilishandanishwa na kampuni nyingine na hatimaye ikashinda,” alisema Mhando.

No comments:
Post a Comment