Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya
ARSENAL YANASA KIFAA CHA HISPANIA KILICHOTWAA NDOO YA EURO 2012
KLABU ya Arsenal ipo karibu kuinasa saini ya Mspanyola Santi Cazorla, mwenye umri wa miaka 27, baada ya kiungo huyo wa Malaga kukubaliana vipengele na The Gunners.
Joe Allen, mwenye umri wa miaka 22, anaweza kuondoka Swansea kwa dau la pauni Milioni 15, lakini atahamia klabu za 'top five' club, ikiwemo Liverpool.
KLABU ya Paris Saint-Germain iko tayari kuipiga bao Real Madrid katika kuwania saini ya kiungo wa Tottenham, Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26.
KLABU ya Tottenham imeishambulia Arsenal kwa kucheza rafu katika kuwania saini ya kipa Mfaransa, Hugo Lloris, mwenye umri wa miaka 25, ambaye Spurs wanamtaka pia.
Spurs inamtaka mchezaji ambaye muda mrefu Chelsea wanamtaka, kiungo wa Shakhtar Donetsk, Willian, mwenye umri wa miaka 23.
Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 19, anabaki Sao Paulo na hatakwenda Manchester United, kwa mujibu wa wakala wa Mbrazil huyo.
Rais wa Sao Paulo, Juvenal Juvencio anataka kumbakiza klabu hapo Moura, kwa mujibu wa taarifa nchini Brazil.
Man United itajaribu kwa mara mwisho kumpata Moura au itaamua kuachana na mpango huo moja kwa moja.
AC Milan inataka kuanza mazungumzo na Manchester City juu ya uwezekano wa kumsajili Muargentina, Carlos Tevez, mwenye umri wa miaka 28.
BEKI wa Manchester City, Aleksandar Kolarov yupo karibu kurejea Serie A wakati Inter Milan inatazamiwa kukamilisha uhamisho wa pauni Milioni 6.2.
Oscar, mwenye umri wa miaka 20, anakaribia kutua Chelsea kwa mujibu wa rais wa klabu ya Internacional, Giovanni Luigi, ambaye amesema mazungumzo yamefikia pazuri.
KLABU ya AS Roma iko mbele ya Chelsea na Manchester United katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa Benfica, Axel Witsel, mwenye umri wa miaka 23.
Newcastle imepuuza madai kwamba Rubin Kazan inajiandaa kumsajili Demba Ba, mwenye umri wa miaka 27.
BEKI wa Everton, Johnny Heitinga, mwenye umri wa miaka 28, anajiandaa kwenda Uturuki katika klabu ya Fenerbahce kwa dau la uhamisho la pauni Milioni 5 katika siku chache zijazo baadaye.
OTHER GOSSIP
Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 23, anaweza kucheza Tottenham kabla ya Team GB haijacheza mechi yake ya kwanza ya Olimpiki, licha ya kutemwa kwenye kikosi cha Stuart Pearce kwa sababu ya majeruhi.
MATUMAINI ya Liverpool kumsajili Nahodha wa Poland, Jakub Błaszczykowski, mwenye umri wa miaka 26, yameota mbawa baada ya winga huyo wa Borussia Dortmund kusaini mkataba mpya wa miaka na klabu yake, mabingwa wa Ujerumani.
AC MILAN KURUDISHA TIKETI...
AC Milan imesema itarudisha tiketi za msimu ambazo zimeuzwa msimu huu, kufuatia kuuzwa kwa wachezaji wawili nyota Zlatan Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 30 na Thiago Silva, mwenye miaka 27, kwenda Paris Saint-Germain.
No comments:
Post a Comment