Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’.
Lile sakata la bosi wa Chuz Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’
kudaiwa kuingia mitini na ‘mafweza’ ya ndugu wa Rais Joseph Kabila wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Itien Kabila kiasi cha Sh. milioni 500
limefungukia ukurasa mwingine ambapo mwigizaji ‘seksi’ Bongo, Halima
Yahya ‘Davina’ anadaiwa kufahamu mchongo mzima.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Davina ndiye mtu wa kati katika sakata hilo ambapo yeye alikuwa shahidi wa Chuz kukopeshwa kiasi hicho cha fedha na alikula kitu kidogo kama ‘macho kuona’.
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Davina na kumuuliza kama taarifa hizo zina ukweli wowote ambapo aliruka kimanga akisema: “Akha! Mi simjui huyo Kabila, nani kawaambia?”
Chuz alipopigiwa simu juzi Jumamosi na kuulizwa kuhusu ushiriki wa Davina, alikiri kufahamu yeye kukopeshwa fedha hizo lakini akasema msanii huyo si shahidi wala hakulipwa fedha yoyote.
Aliongeza: “Lakini mbona mmekomalia ishu ambayo hainihusu, kuna nini kwani jamani? Yeye si kasema ataizuia filamu yangu ya Dirty Game, afanye hivyo kama ana ubavu.”
No comments:
Post a Comment