Tuesday, July 24, 2012

UNITED YAGONGA MWAMBA TENA KWA MOURA.

 
 Lucas Moura.
Matumaini ya meneja wa klabu ya Manchester United kumsajili Lucas Moura kwa paundi milioni 30 yamefutika baada ya klabu hiyo kuonywa kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil hawezi kuondoka katika klabu yake ya Sao Paulo. Akiwa tayari amewasajili Shinji Kagawa na Nick Powell katika kipindi hiki
cha majira ya kiangazi, Ferguson alikuwa na matumaini ya kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 kwa hela nyingi. Lakini Ferguson amechanganywa na suala la uhamisho wa Moura ambaye kwasasa yuko jijini London na kikosi cha Brazil kwa ajili michuano ya Olimpiki baada ya kukataliwa kwa mara ya pili sasa. Wakala wa Moura, Wagner Ribeiro sasa amepigilia msumari wa mwisho katika jeneza la United baada ya kusisitiza kinda huyo anahitajia kiasi cha fedha ambacho timu hiyo haiwezi kufikia hivyo atabakia katika klabu yake ya Sao Paulo.

No comments: