Usain Bolt.
Mwanarihadha nyota wa mbio fupi, Usain Bolt anajiandaa kuvunja rekodi yake mwenyewe tena kwa kukimbia mita 100 kwa kutumia sekunde 9.4 lakini akasema kuwa huo ndio utakuwa mwisho. Kocha wake Glen Mills siku zote amekuwa akitabiri kuwa Bolt atakuwa katika kiwango bora zaidi wakati atapotimiza miaka 26 ambayo ataitimiza katika kipindi cha wiki mbili baada ya kumalizika kwa michuano Olimpiki.
Akiwa ameweka rekodi ya dunia ya sekunde 9.58 katika mbio za mita 100 na sekunde 19.19 katika mbio za mita 200 na kuondoka na medali ya dhahabu katika mashindano ya dunia yaliyofanyika jijini Berlin mwaka 2009, Bolt bado amesisitiza anaweza kufanya vizuri zaidi hapo. Afya ya Bolt imekuwa ikiwaogopesha mashabiki wake katika michuano ya olimpiki huku mpinzani wake mkubwa kwenye mbio Yohan Blake ambaye wanafundishwa na kocha mmoja akipewa nafasi ya kumpa wakati mgumu Bolt. Lakini Bolt amekuwa akijiamini kufanya vizuri katika michuano hiyo akidai kuwa naweza kukimbia kwa kutumia sekunde 9.4 ingawa hata hivyo alidai haitawezekana kwa mtu yeyote kukimbia chini ya hapo. Bolt amesema kuwa hakuna binadamu wa kawaida anayeweza kukimbia kwa kutumia sekunde 9.2 hata kama atafanya mazoezi makali kiasi gani na kutumia mbinu zozote zinazohitajika.
No comments:
Post a Comment