Tuesday, July 24, 2012

JOHARI AFUNGUKA.

 
Johari.
Kinara wa filamu za kibongo Johari, alifunguka kuwa anatarajia kuitoa filamu mpya inayokwenda kwa jina la ‘Ramadhani Kareem’, ambayo itakuwa kama zawadi kwa mashabiki wake waliofunga mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Wakati akiizungumzia filamu hiyo Johari, alidai kuwa ndani ya kazi kutakuwa na wasanii wengine kama   
Ray, Chuchu Hans, Lisa, na wasanii wengine kibao.
Alisema kuwa filamu hiyo itahusu mwezi mtukufu pekee kwani itafundisha mambo mengi yanatakayowapa faraja watu wote waliofunga kwa ajili ya kumuomba mwenyezi mungu.
“Sina filamu nyingine kwa sasa zaidi hii ambayo ni zawadi kwa mshabiki wangu, kwani itazungumzai sana juu ya mwezi huu mtukufu ambayo watu wengi wa dini wa Kiisilamu wanakuwa wamefunga,” alisema.
Aliuongeza kuwa kazi hiyo itakuwa inatazamwa kila mwaka kwani kipindi mfungo si cha mwaka mmoja pekee hivyo mashabiki wake wataendelea kuitazama filamu hiyo miaka yote.

No comments: