Tetesi za Jumapili magazeti Ulaya
NEWCASTLE YAMRUDIA ANDY CARROLL
KLABU ya Newcastle itarefufua nia yake ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll baada ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 kusema ataondoka Anfield ili apate furaa ya kucheza michuano ya Ulaya.
Lakini Newcastle itamrejea mshambuliaji wake huyo wa zamni iwapo tu itamuuza mshambuliaji wake mwenye thamani ya pauni Milioni 7, Demba Ba, 27.
KLABU ya Arsenal inatarajia kukamilisha uhamisho wa pauni Milioni 15 wa kiungo wa Malaga, Santi Cazorla, mwenye umri wa miaka 27 Jumanne.
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini anaamini mabingwa wa Ligi Kuu watatangaza wachezaji wao wapya, iliyowasajili muda si mrefu ujao.
KOCHA wa West Brom, Steve Clarke amethibitisha kwamba mshambuliaji Shane Long, mwenye umri wa miaka 25, hauzwi, baada ya Reading kuonyesha nia ya kumsajili.
KLABU ya Fulham iko tayari kuomba kumsajili kiungo wa kimataifa wa Urusi, anayechezea Arsenal, Andrey Arshavin, mwenye umri wa miaka 31, ambaye inaaminika anataka kubaki London.
KLABU ya Manchester City inaweza kumkosa mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28, bdaada ya kiongozi wake, Brian Marwood kughairi kumfanya awe mchezaji ghali katika klabu hiyo.
WAKALA aliyefanikisha mpango wa mshambuliaji Emmanuel Adebayor kutoka Arsenal kwenda Manchester City anaamini mshambuliaji huyo hapendi kuhamia to Tottenham.
SCHOLES ALIKUWA TAYARI KURUDI ENGLAND
KIUNGO wa Manchester United, Paul Scholes angeweza kurejea kwenye kikosi cha England kilichocheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, lakini hakupigiwa simu na kocha wa timu hiyo, Roy Hodgson.
VERMAELEN AZINGUANA NA REFA...
NYOTA wa Arsenal, Thomas Vermaelen alizinguana na refa msaidizi, Sian Massey katika mechi ambayo timu yake ilifungwa 2-0 na Manchester City mjin Beijing, China.
No comments:
Post a Comment