Sunday, July 29, 2012

SPIDER MAN MFUNGAJI BORA KAGAME.

 

 Said Bahanuzi, mshambuliaji mpya wa Yanga, kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, ndiye mfungaji bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuwapiku John Raphael Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC, Hamisi Kiiza ‘Diego’ wa Yanga pia na Taddy Etikiama na AS Vita ya DRC.
Bahanuzi amemaliza na mabao sita sawa na Taddy, lakini kwa kuwa mshambuliaji wa Vita bao lake moja ni la penalti, alilofunga kwenye mechi ya Kundi A na Simba katika sare ya 1-1, kiatu cha Dhahabu amepewa Side Ba.
Hamisi Kiiza alipewa kimakosa bao moja awali, ambalo lilikuwa la beki wa Yanga, Stefano Mwasyika na sasa amemaliza na mabao matano sawa na Adebayor wa Chamazi.
Suleiman Ndikumana wa APR amemaliza na mabao matatu, Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ wa Simba SC amemaliza na mabao mawili sawa na Leonel St Preus wa APR, Didier Kavumbagu wa Atletico, Feni Ali na Robert Ssentongo wa URA.
 

WAFUNGAJI BORA KAGAME 2012:
Said Bahanuzi                  Yanga SC    6
Taddy Etikiama                 AS Vita        6-1
Hamisi Kiiza                      Yanga SC    5
John Bocco                       Azam FC     5
Suleiman Ndikumana        APR             3
Abdallah Juma                  Simba SC    2
Leonel St Preus                APR             2
Didier Kavumbagu            Atletico         2
Feni Ali                             URA             2
Robert Ssentongo             URA             2

No comments: