Didier Kavumbangu.
Mshambuliaji
wa Atleticon ya Burundi, Didier Kavumbangu (pichani) amesaini Yanga
juzi. Kiongozi Mkuu wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Seif Ahmad 'Magari' ametangaza leo kwamba wamemsajili mchezaji huyo na
sasa
wameimarisha safu yao ya ushambuliaji, yenye wakali wengine kama Hamisi
Kiiza na Said Bahanuzi. Kavumbangu ndiye aliyefunga mabao yote mawili
katika mchezo wa kwanza wa Kundi C, Yanga ikilala 2-0 mbele ya Atletico,
mchezo pekee mabingwa hao wa Kagame kufungwa mashindano ya mwaka huu.
No comments:
Post a Comment