Wednesday, July 25, 2012

NMB YACHANGIA MILIONI 1O/- KWA WAATHIRIKA WA AJALI YA MV SKAGIT.

Mkurugenzi Mkuu wa Kamati ya Maafa Zanzibar, Bw. Ali Juma Hamad (Kushoto), akipokea sehemu ya msaada kutoka kwa Meneja wa Tawi wa Benki ya NMB Zanzibar, Bw. Mluku Abdallah Maggid, kisiwani Unguja .Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 10/- ni maalum kufuatia maafa ya ajali ya MV Skagit iliyotokea Julai 18, mwaka huu.
Maafisa wa Benki ya NMB tawi la Zanzibar wakibeba vifaa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Ali Seif Idd (Kati), akizungumza na Meneja wa Tawi la Benki ya NMB Zanzibar, Mluku Abdallah Maggid ofisini kwake kisiwani humo wakati akipokea msaada huo. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed.

No comments: