Mrisho Ngassa akiwa katika Benchi la Azam katika mechi ya robo fainali kombe la Kagame kati ya Azam na Simba.Kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amesema hamtumii Mrisho Khalfan Ngassa kwa sasa, kwa sababu haonyeshi dalili za kutaka kucheza.
“Hana jitihada zozote, hajitumi, hana hamu ya kucheza, siwezi kumchezesha,”alisema Stewart
mapema tu, kabla ya mechi ya Robo Fainali dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pamoja na kucheza bila Ngassa, Azam imeshinda 3-1 na kuingia Nusu Fainali, ambako itamenyana na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kuna tetesi kwamba, Ngassa yupo kwenye mgomo baridi kushinikiza uhamisho wa kurejea Yanga, lakini habari ambazo zimepatikana kutoka ndani ya Azam, zinasema kwamba, klabu hiyo itaendelea kuishi naye hivyo hivyo ‘kimakunyanzi’ hadi amalize mkataba wake msimu ujao.

No comments:
Post a Comment