
Timu ya taifa ya vijana
chini ya miaka 23 ya Hispania imeenguliwa mapema katika michuano ya
Olimpiki inayofanyika jijini London baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0
kutoka kwa Honduras ikiwa ni kipigo cha pili mfululizo kufuatia kile
walichopata kutoka kwa Japan kwa idadi kama hiyo ya mabao. Honduras
ambao walishinda bao la mapema kupitia kwa mshambuliaji wake Jerry
Bengtson wamefanikiwa kutinga hatua ya
robo fainali pamoja na Japan
ambao waliwafunga Morocco bao 1-0 katika kundi D. Katika
michezo ya kundi C Brazil ilifanikiwa kusonga mbele baada ya kuifunga
Belarus mabao 3-1 wakati Misri ilitoa sare ya bao 1-1 na New Zealand
hivyo itabidi washinde mchezo wao wa mwisho dhidi ya Belarus ili waweze
kusonga mbele. Mexico
ilifanikiwa kushinda mabao 2-0 dhidi ya Gabon katika kundi B wakati
Korea Kusini walifanikiwa kushinda mabao 2-1 hivyo kupelekea timu hizo
kuwa na alama sawa katika kundi hilo.
No comments:
Post a Comment