
Dereva wa magari yaendayo
kasi ya Langalanga kutoka timu ya McLaren, Lewis Hamilton amefanikiwa
kushinda mbio za Hungary Grand Prix jana. Hamilton
ambaye ni raia wa Uingereza alimaliza mbio hizo kwa kasi zaidi ya
wenzake ambao aliwaacha kwa sekunde 0.413 na kufuatiwa na dereva wa timu
ya Lotus,
Romain Grosjean aliyeshika nafasi ya pili katika mbio hizo. Sebastian
Vettel wa timu ya Red Bull alimaliza katika nafasi ya tatu akifutiwa na
Jenson Button ambaye ni muingereza kutoka timu ya McLaren pia alimaliza
katika nafasi ya nne. Wengine
ni Kimi Raikkonen aliyemaliza katika nafasi ya tano akifuatiwa na
Fernando Alonso wa timu ya Ferrari katika nafasi ya sita wakati mkali
mwingine wa mbio hizo Mark Webber alimaliza katika ya 11. Magari
ya Ferrari ambayo yalitamba kipindi cha mvua katika michuano ya
Ujerumani katika mbio hizo za majira ya kiangazi yameshindwa na
kusababisha kupunguza pengo la alama ambazo Alonso alikuwa akiongoza
katika orodha ya madereva bora duniani.
No comments:
Post a Comment