
Jack Wilshere.
Meneja wa klabu ya
Arsenal Arsenal Wenger amesema kuwa kiungo nyota wa klabu hiyo Jack
Wilshere hata kuwa sehemu ya kikosi chake katika michezo ya mwanzo wa
Ligi Kuu nchini Uingereza kutokana na majeraha yanamsumbua. Wilshere
ambaye ana miaka 20 alishindwa kucheza msimu uliopita kutokana na
kufanyiwa upasuaji wa goti aliofanyiwa Mei mwaka jana. Wenger
ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukamilisha
ziara ya bara la Asia jijini Hong Kong amesema kuwa anatarajia mchezaji
huyo kurejea dimbani mwezi Octoba. Wakati
akiuguza goti lake Wilshere alilitonesha tena wakati akifanya mazoezi
ili arejee uwanjani na hivyo kumfanya mchezaji kukosa michuano ya Ulaya
iliyomalizika Julai mosi mwaka huu ambapo anatarajiwa kuanza mazoezi
mepesi Agosti na akitarajia kurejea uwanjani Octoba.
No comments:
Post a Comment