Tuesday, July 24, 2012

KOSCIELNY AJITIA KITANZI ARSENAL.

Laurent Koscielny.
Beki wa klabu ya Arsenal, Laurent Koscielny amekubali kusaini mkataba wa muda mrefu na klabu hiyo yenye maskani yake kaskazini mwa jiji la London, Uingereza. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye ana umri wa miaka 26 amejitengenezea nafasi katika kikosi cha kwanza kwenye klabu hiyo kutokana na kiwango bora ambacho amekuwa akionyesha toka alipojiunga miaka miwili iliyopita. Uamuzi wa beki huyo umekuja baada ya mshambuliaji
nyota wa kimataifa wa Uholanzi, Robin van Persie kutangaza kuwa hataki kusaini mkataba mwingine. Mkataba wa sasa wa Van Persie unaisha mwishoni mwa msimu ujao na mchezaji huyo amedai kuwa anataka changamoto nyingine baada ya miaka nane ya kuitumikia klabu hiyo. Meneja wa klabu hiyo, Arsenal Wenger amesema kuwa hatma ya mchezaji huyo iamuliwe kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi inayotarajiwa kuanza Agosti 18 mwaka huu huku klabu za Manchester United, Manchester City na Juventus ambazo zote zimekuwa zikimuhitaji.

No comments: