Kiungo wa zamani wa Simba SC, Issa Kihange amefariki dunia
jana maeneo ya nyumbani kwake, Mbezi Jogoo, baada ya kuanguka uwanjani wakati
akicheza mechi za maveterani.
Kwa mujibu wa kiungo wa zamani wa Yanga, Waziri Mahadhi ‘Mandieta’
aliyekuwapo maeneo ya tukio, alisema kwamba baada ya Kihange kuanguka wakati
akishangilia bao alilofunga mazoezini uwanjani, alikimbizwa hospitali ya IMTU,
ambako umauti ulimfika.
Issa Kihange alikuwamo na aling’ara kwenye kikosi cha Simba
kilichotwaa taji la pili Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame
mwaka 1991 mjini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment