Shirikisho la Soka
barani Ulaya-UEFA limekipiga faini ya euro 25,000 Chama cha Soka cha
Ujerumani-DFB kutokana na tabia isiyofaa iliyoonyeshwa na mashabiki wa
timu ya taifa ya nchi hiyo wakati wa mchezo wa kundi B ambapo Ujerumani
ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Denmark Juni 17 mwaka huu. Mashabiki wa
nchi hiyo walikuwa wakiwasha mafataki na
kuonyesha mabango ambayo
hayaruhusiwi katika michuano hiyo ambayo yanachochea ubaguzi katika
mchezo wa soka. Faini hiyo inakuwa sio ya kwanza kwa DFB ambapo tayari
walishatozwa faini ya euro 10,000 wakati mashabiki wa Ujerumani
waliporusha karatasi ambao walikuwa wameikunja mfano wa ndizi kwa
wachezaji wa Ureno katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa June 9
jijini Lviv. Ujerumani ambao wameshinda michezo yao yote minne
waliyocheza na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ambapo
watakutana na Italia katika Uwanja wa Taifa jijini Warsaw, Poland,
wanaweza kukata rufani kupinga adhabu hiyo lakini inatakiwa iwasilishwe
ndani ya masaa 24.
No comments:
Post a Comment