Kiungo wa kimataifa wa
Ufaransa, Samir Nasri huenda akafungiwa kucheza michezo ya kimataifa kwa
miaka miwili baada ya kumshambulia mwandishi wa habari katika michuano
ya Ulaya mwaka huu. Kiungo huyo alikwaruzana na mwandishi wa Ufaransa
baada ya timu hiyo kung’olewa
katika robo fainali ya michuano ya Ulaya
baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Hispania.
Nasri ambaye
aliingia katika mchezo huo kama mchezaji wa akiba alimjibu mwandishi
huyo kwa lugha chafu baada ya kuulizwa swali kuhusiana na mchezo huo
mara baada ya kumalizika. Hiyo inakuwa ni mara ya pili kwa mchezaji huyo
kuingia katika mzozano na mwandishi huyo ambapo mara kwanza
alishangilia bao akimwambia mwandishi huyo kufunga mdogo wake wakati
alipofunga bao ya kusawazisha dhidi ya Uingereza katika mchezo wa
ufunguzi wa kundi D dhidi ya Uingereza. Rais wa Shirikisho la Soka la
Ufaransa-FFF, Noel le Graet amesema kuwa tukio alilofanya mchezaji huyo
halivumiliki na kumuonya Nasri kuwa anapaswa kuzuia hasira zake katika
siku mbeleni.
No comments:
Post a Comment