Jakob Michelsen.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limemtambulisha rasmi leo mbele ya waandishi wa habari kocha mpya
wa timu za Taifa za vijana, Jakob Michelsen kutoka Denmark ambaye
amechukua nafasi ya Kim Poulsen ambaye hivi sasa anainoa Taifa Stars.
Michelsen ambaye amepewa mkataba wa
mwaka mmoja alitambulishwa na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah na
kusema falsafa yake ni kama ile ya Poulsen ya kumiliki mpira na
kushambulia muda wote wa mchezo.
Kabla ya kuja Tanzania, Michelsen
alikuwa kocha wa timu ya daraja la kwanza ya Hobro IK ya Denmark. Ana
leseni A ya ukocha kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA),
leseni ya ukocha wa vijana kutoka Chama cha Mpira wa Miguu cha Denmark
(DBU).
Moja ya mafanikio yake ni kuipa
ubingwa wa Denmark, timu ya Skovbakken kwenye ligi ya timu zenye umri
chini ya miaka 18. Ubingwa huo aliupata msimu wa 2005/2006.
No comments:
Post a Comment