Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya



VAN PERSIE DILI LINGINE LATUA ARSENAL

KLABU ya Paris Saint-Germain imeungana na Manchester City katika mbio za kuwania saini ya Nahodha na mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie.
BEKI wa Liverpool, Martin Skrtel amezikaushia tetesi za kumhusisha na mpango wa kuhamia Manchester City.
MCHEZAJI anayetakiwa na Tottenham, Nuri Sahin amegoma kwenda kuziba pengo la Luka Modric akisema kwamba anafurahia maisha na anapenda kubaki Real Madrid.
KOCHA wa Ajax, Frank de Boer amewaambia Tottenham wasikate tamaa ya kumsajili beki Jan Vertonghen, licha ya kutofautiana na klabu hiyo ya Uholanzi.
Wayne Rooney
Guangzhou Evergrande iko tayari kumsajili Wayne Rooney
MABINGWA wa Ligi Kuu ya China, Guangzhou Evergrande wameripotiwa kutaka kuwanunua kiungo wa Real Madrid, Kaka na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
KLABU ya Liverpool imeangukia kwenye vumbi katika mbio za kuwania saini nyota wa kimataifa wa Uruguay, Gaston Ramirez baada ya kuzidiwa kete na Juventus.
KLABU bingwa Ulaya, Chelsea itakutana na upinzani mkali kutoka kwa Napoli katika kuwania huduma ya beki wa pembeni wa Porto, Alvaro Pereira.
KLABU ya Newcastle itarudi kwa klabu ya Lille ikiwa na dau lililonenepeshwa kidogo hadi pauni Milioni 6, kwa ajili ya kutaka kumnunua beki wa kulia wa Ufaransa, Mathieu Debuchy.
NEWCASTLE 'The Magpies' pia wanataka kusajili kinda la miaka 19, beki Curtis Good kutoka klabu ya Australian, Melbourne Heart, kwa dau la uhamisho wa pauni 400,000. Habari kamili: Goal.com 
MCHEZAJI anayetakiwa na klabu za Arsenal na Tottenham, Samir Handanovic hauzwi sasa hivi, kwa mujibu wa Meneja wa Udinese, Andrea Carnevale.
Modibo Maiga
Modibo Maiga anayetakiwa na  West Ham
KLABU za Fulham, Norwich na West Brom zipo katika njia tatu tofauti kuwania saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Denmark, Nicklas Helenius, ambaye aling'ara akiwa na Aalborg msimu uliopita.
KOCHA Sam Allardyce anatarajiwa kuimarisha kikosi chake katika safu ya ushambuliaji West Ham kwa kukata dau la pauni Milioni 5 ili kumnasa mshambuliaji wa Sochaux, Modibo Maiga.
KLABU ya Sunderland inamuwania beki wa Aston Villa, Carlos Cuellar.
KLABU ya Fulham inamtaka kiungo wa Tottenham, David Bentley, ama kwa mkopo au kumbeba jumla.
KLABU ya Southampton imeungana na Fulham na QPR katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa Vitesse Arnhem, Alexander Buttner.
KLABU ya Wolves iko tayari kumtwaa beki wa Manchester City, Stefan Savic kwa mkopo.
Cristiano Ronaldo
Kwa nini Ronaldo hakupiga penalti ya kwanza?

EURO 2012

LUIS Nani amesema mchezaji mwenzake wa Ureno, Cristiano Ronaldo alielekezwa akapige penalti ya ushindi katika Nusu Fainali ya Euro 2012 juzi dhidi ya Hispania, ambao walishinda kabla ya nyota huyo wa Real Madrid hajaenda kupiga.
RONALDO amesema kwamba kocha Paulo Bento hakuwa na jinsi zaidi ya kumteua yeye kupiga penalti ya mwisho.

SEEDORF SPURS AU LA GALAXY?

MCHEZAJI anayetakiwa na Tottenham, Clarence Seedorf bado anafikiria kwenda kumalizia soka yake LA Galaxy.
BEKI Ledley King atafanyiwa vipimo vya goti lake mwanzoni mwa msimu, lakini atapewa ofa ya ukocha ikiwa atakataa kusaini mkataba mpya Tottenham.
LICHA ya kuonekana yuko 'ovyo' katika kikosi cha England kwenye Euro 2012, Wayne Rooney ameambiwa hana sababu ya kwenda na klabu yake, Manchester United katika ziara ya kujiandaa na msimu mpya, Afrika Kujsini na China.