Wakali
 wa muziki wa kizazi kipya Mwana FA na Ommy Dimpoz wanatarajiwa 
kumsindikiza chipukizi mkongwe kwenye muziki wa kizazi kipya Bi Kidude 
kwenye maonyesho yake matatu Mkoani Mwanza. Maonyesho hayo yatafanyika 
kuanzia Julai sita, saba na nane, katika kumbi mbalimbali mkoani Mwanza.
Ziara hiyo imepewa jina la usiku wa mtu mzima dawa likiandaliwa na 
Meneja wa TMK Family, Said Fella. Fella aliliambia Blog hii kuwaonyesho 
la kwanza litafanyika Julai 6 (Ijumaa) katika Ukumbi wa Villa Park, 
jijini Mwanza.
Maonyesho mengine yatafanyika Julai 7 (Jumamosi) kwenye Ukumbi wa Ambassador Club uliyopo Geita na lile onyesho la mwisho litakuwa Jumapili ya Julai 8 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Wasanii wengine watakaokuwemo kwenye ziara hiyo ya mtu mzima dawa, itakuwa wakali wote kutoka TMK Family kama Temba, Chegge na Aslay.

No comments:
Post a Comment