Tuesday, June 26, 2012
URUSI, HISPANIA ZAWEKWA KIKAANGONI KUFUATIA TUHUMA ZA UBAGUZI.
Shirikisho la soka
barani Ulaya-UEFA imezifungulia mashtaka vyama vya soka vya Hispania na
Urusi kutokana na matukio ya kibaguzi yaliyoonyeshwa na mashabiki wa
timu zao za taifa katika michuano ya Ulaya inayoendelea nchini, Poland
na Ukraine. Mashtaka hayo yamekuja kufuatia taarifa kuwa kulikuwa na
baadhi ya mashabiki Hispania wakipiga kelele za nyani kumlenga
mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli huku mashabiki wa Urusi wakiwa
wamemlenga beki wa Jamhuri ya Czech Theodor Gebre Selassie katika
michezo ambayo timu hizo zilikutana. Shirikisho hilo limesema kuwa
limefungua kesi za utovu wa nidhamu zilizoonyeshwa na mashabiki hao
ambapo bodi ya kupambana na uaguzi katika mchezo wa soka barani Ulaya
itakutana Alhamisi kushughulikia suala hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment