Miki Roque.
Beki wa zamani wa
Liverpool Miki Roque amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 23 jijini
Barcelona, Hispania kufuatia kusumbuliwa na maradhi ya saratani. Beki
huyo ambaye mpaka mauti yanamkuta alikuwa akikipiga katika klabu ya Real
Betis alianza katika timu ya vijana ya Liverpool kuanzia mwaka 2005
mpaka 2009 na kufanikiwa kushinda Kombe la Vijana la
FA mwaka 2006 kabla
ya kujiunga na Betis. Amewahi kucheza mara moja katika kikosi cha
kwanza cha Liverpool katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Desemba
mwaka 2006 dhidi ya timu ya Galatasaray. Roque aligundulika kuwa na
saratani mapema mwaka jana ambapo alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe
katika fupanyonga lakini matibabu hayo hayakuzaa matunda kwani mchezaji
huyo aliendelea kupambana na maradhi hayo mpaka mauti yalipomkuta
Jumamosi iliyopita. Klabu ya Liverpool imetuma salamu za rambirambi kwa
familia ya mchezaji huyo na kumuelezea kwamba alikuwa mchezaji kijana
mwenye upendo na juhudi kubwa awapo uwanjani.
No comments:
Post a Comment