Cuneyt Cakir.
Shirikisho la Soka
barani Ulaya-UEFA limetangaza majina ya waamuzi watakaochezesha michezo
ya nusu fainali ya michuano ya Ulaya itakayochezwa Jumatano na Alhamisi
ya wiki hii. Mwamuzi Cuneyt Cakir kutoka Uturuki ndio anatarajiwa
kuchezesha mchezo kati ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo Hispania
dhidi ya Ureno mchezo ambao unatarajiwa
kupigwa jijini Donetsk, Ukraine
kesho kutwa. Wakati Stephane Lannoy kutoka Ufaransa yeye atachezesha
mchezo baina ya Ujerumani ambao watakuwa wakijaribu kufikia hatua ya
fainali ya michuano hiyo baada ya kushindwa kutamba mbele ya Hispania
mwaka 2008 dhidi ya Italia mchezo utakaochezwa jijini Warsaw, Poland.
Italia wametinga hatua hiyo baada ya kuwaondoa kwa changamoto ya mikwaju
ya penati Uingereza baada ya timu hizo kushindwa kufungana katika muda
wa kawaida wakati Ujrumani wao waliingia kwa kishindo katika hatua hiyo
baada ya kuifunga Jamhuri ya Czech mabao 4-2.
No comments:
Post a Comment