Taoufik Makhloufi.
Mwanariadha nyota kutoka
Algeria, Taoufik Makhloufi amefanikiwa kushinda medali ya dhahabu katika
mbio za mita 1500 ikiwa ni taji lake kubwa la kwanza. Makhloufi
ambaye ana umri wa miaka 24 alimaliza mbio hizo akitumia muda wa dakika
tatu na sekunde 34.04 akiwazidi Leonel Manzano wa Marekani
ambaye
alinyakuwa medali ya fedha akitumia muda wa dakika tatu na sekunde 47.79
na Abdalaati Iguider wa Morocco akinyakuwa medali ya shaba. Bingwa
mtetezi wa mbio hizo Asbel Kiprop kutoka Kenya alishika nafasi ya
mwisho katika mbio hizo kutokana na kupata maumivu ya misuli. Makhloufi
abaye alifika hatua ya nusu fainali katika michuano ya dunia ya mbio
hizo iliyofanyika jijini Daegu alikuwa akichuana vikali na Kiprop ambaye
ni bingwa wa michuano hiyo iliyofanyika jijini Beijing lakini alipoumia
Mualgeria huyo alijiweka katika nafasi nzuri na kuhakikisha anamaliza
wa kwanza.
No comments:
Post a Comment