
WACHEZAJI 21 WATEULIWA KIKOSI CHA TAIFA STARS.
Kocha Mkuu wa Taifa
Stars, Kim Poulsen leo (Agosti 1 mwaka huu) ametangaza kikosi cha
wachezaji 21 kwa ajili ya mechi ya kirafiki itakayochezwa ugenini Agosti
15 mwaka huu. Wachezaji walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambi kwenye hoteli ya
Tansoma, Dar es Salaam, Agosti 8 mwaka huu saa 1 jioni tayari kwa
mazoezi yatakayoanza siku inayofuata. Makipa
walioitwa kwenye kikosi
hicho ni Deogratias Munishi (Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na
Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha msaidizi Aggrey Morris (Azam),
Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe
(Simba). Viungo ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna
Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan
Chombo (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar). Wachezaji wanaounda safu ya ushambuliaji
ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
No comments:
Post a Comment