
Yen Shuwen.
Muogeleaji kinda kutoka
China Yen Shiwen ameshinda medali yake ya pili ya dhahabu ya mita 200
katika michuano ya kuogelea ya Olimpiki inayoendelea jijini London.
Shiwen mwenye umri wa miaka 16 ambaye alishinda medali ya dhahabu pia
katika mashindano hayo ya mita 400 kwa kutumia muda wa dakika 7.57 na
kuweka rekodi ya muda wa kasi zaidi katika michuano hiyo. Katika
mashindano hayo Alicia Coutts alishika nafasi ya pili na kupewa medali
ya fedha akitumia muda wa dakika 2.08.15 wakati Caitlin Leverenz wa
Marekani alishinka nafasi ya tatu na kupata medali ya shaba akitumia
muda wa dakika 2.08.95. Katika michuano hiyo China inaongoza kwa
kunyakuwa medali nyingi zaidi ikiwa imejikusanyia medali 23, dhahabu 13
fedha sita na shaba nne, nchi inayofuatia ni Marekani nayo ikiwa na
idadi sawa ya medali 23 lakini wenyewe wakiwa na dhahabu tisa fedha nane
na shaba sita. Nchi ya tatu kwa wingi wa medali mpaka sasa ni Ufaransa
ambayo imenyakuwa medali 11, medali nne za dhahabu, tatu za fedha na nne
za shaba.
No comments:
Post a Comment