Floyd Mayweather akitolewa gerezani na walinzi kutoka gereza hilo la Las Vegas, baada ya kumaliza kifungo chake.
Bondia ambaye hajawahi kupigwa katika ngumi za kulipwa, Floyd Mayweather
ametoka jela juzi na anaonekana yuko fiti kabisa, mwenye afya njema na
misuli ya nguvu baada ya kutoka ndani ya gereza la Clark County Jail,
alikowekwa miezi miwili iliyopita. Bondia huyo sasa anaweza kupata
ulingoni Novemba 8, mwaka huu kumaliza ubishi na mpinzani wake wa siku
nyingi, Manny Pacquiao, pambano ambalo anaweza kulipwa dola za
Kimarekani Milioni 200.
Mayweather akitabasamu wakati akilakiwa na marafiki na familia yake baada ya kutolewa jela. |
Hii ni picha ambayo ameiweka kwenye twitter, cheki anavyoonekana. |
No comments:
Post a Comment