Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya


ARSENAL WAIFANYIA UNOKO MAN UNITED KWA VAN PERSIE WAKIUGULIA MAUMIVU YA LUCAS MOURA KUWAPONYOKA

Arsenal haitamuuza Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 29, kwa dau la chini ya pauni Milioni 20 na itataka Pauni Milioni 5 zaidi, ikiwa Manchester United watatoa ofa ya kumnunua mshambuliaji huyo.
Joe Allen
Allen alikuwa moja ya bidhaa adimu kwa Brendan Rodgers alipokuwa Swansea
Mpango wa Manchester United kumsajili  Lucas Moura umekufa rasmi baada ya kinda huyo wa miaka 19 kutoka Brazil kukubali mkataba wa miaka minne na nusu na Paris Saint Germain ya Ufaransa.
Brendan Rodgers yu karibu kuungana tena na Joe Allen baada ya Liverpool kutenga dau la pauni Milioni 15 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka  22 wa Swansea City.
Liverpool inamtaka kwa mkopo Adam Johnson mbali na kumuuza kwa pauni Milioni 23 Daniel Agger kwenda Manchester City.
AC Milan inajiandaa kukabiliana na upinzani wa Arsenal na Liverpool katika kuwania huduma ya kiungo wa Real Madrid, Nuri Sahin, mwenye umri wa miaka 23, ambaye Jose Mourinho amemruhusu kuondoka kwa mkopo.
Fernando Llorente
Llorente amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Athletic Bilbao
Mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Fernando Llorente amekataa mkataba mpyya, hivyo kuzipa nafasi ya kumsajili klabu za Chelsea na Liverpool zinazommezea mate mchezaji huyo mwenye umri wa miaka  27.
Tottenham inahusishwa na uhamisho wa kiungo wa Partizan Belgrade, Mohamed Kamara.
Queens Park Rangers inataka kuwasajili wachezaji wawili wa zamani wa Manchester United, kutoka AS Roma beki Gabriel Heinze na Sunderland, Kieran Richardson.
Kocha wa Blackburn Rovers, Steve Kean amesema yu karibu kumnasa kwa mkopo mshambuliaji wa kimataifa wa Uturuki, Colin Kazim-Richards, mwenye umri wa miaka 25, ambaye kwa sasa anachezea Galatasaray.