Tetesi za J'mosi magazeti Ulaya 

MODRIC AUWASHA MOTO SPURS, ATAKA KUJUA MUSTAKABALI WAKE HARAKA

Luka Modric anataka kuzungumza na Andre Villas-Boas juu ya mustakabali wake, na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 anahofia kwamba ndoto zake za kujiunga na Real Madrid zinaweza kuota mbawa.
Adam Johnson
Adam Johnson.
Liverpool inamtaka beki wa Atletico Madrid, Diego Godin, mwenye umri wa miaka 26, azibe pengo la Daniel Agger iwapo Mdenmark huyo atajiunga na Manchester City.
Mchezaji anayewaniwa na klabu za Manchester City na Tottenham, Fernando Llorente, mwenye umri wa miaka 27, anatakiwa pia na Juventus, ambao waliweka dau la pauni Milioni 14, lililopigwa chini na Athletic Bilbao.
Brendan Rodgers anataka kuwasajili Adam Johnson, Nuri Sahin na Clint Dempsey huku Joe Allen akiwa njiani kutua Liverpool akitokea Swansea City.
Manchester City ipo karibu kumsajili beki wa kushoto wa Korea Kusini, Yun Suk-Young, mwenye umri wa miaka 22, kama msaidizi wa Gael Clichy, wakati Aleks Kolarov anatarajiwa kuhama The Blues.
West Ham itatakiwa kuilipa Wolves kiasi cha pauni Milioni 10 kwa ajili ya winga Matt Jarvis, baada ya ofa yao waliyotoa sasa ya pauni Milioni 6 kwa ajili mkimbia pembeni mwa uwanja huyo mwenye umri wa miaka 26, kupigwa chini.
Jermain Defoe, mwenye umri wa miaka 29, yumo kwenye orodha ya wachezaji wanaokwenda Sunderland, baada ya mpango wa Martin O'Neill kujaribu kumsajili Steven Fletcher, mwenye umri wa miaka 25, kutoka Wolves kuonekana kushindikana.
Joey Barton
Joey Barton 
Ian Holloway anataka kumchukua 'Mtukutu' Joey Barton wa QPR mwenye umri wa miaka 29, kwa mkopo wa muda mrefu, baada ya kiungo huyo kuonyesha nia ya kuhamia Blackpool, jirani na kwao, Fleetwood Town.
Fiorentina wana nia ya kumsajili Giovani Dos Santos, mwenye umri wa miaka 23, kutoka Tottenham. Nyota huyo wa Mexico amebakiza chini ya mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa.