Johns Bocco akipambana Mwasika.
Wiki kadhaa baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kagame Cup ambayo aliibuka miongoni mwa wafungaji bora wa michuano hiyo, mchezaji wa kimataifa wa Azam na timu ya taifa ya Tanzania John Bocco amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio ya kwenda kufanya majaribio nje ya nchi.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC, ni kwamba Bocco amepata nafasi ya kwenda South Africa kwa ajili ya kufanya majaribio ya wiki moja.
Taarifa hiyo ilisomeka:
"Azam FC imepokea barua ya mwaliko wa majaribio toka klabu ya Super Sport ya Afrika Kusini kwa mchezaji John Bocco ambapo atapaswa kusafiri Jumamosi tarehe 11/08/2012 kwenda Johannesburg Afrika ya Kusini.
John Bocco atatumia muda wa wiki moja nchini Afrika ya Kusini. Uongozi wa Azam FC unampongeza John Bocco kwa mafanikio haya na unamtakia kila la heri kwenye majaribio yake."
No comments:
Post a Comment