Tetesi za magazeti Jumatano Uaya
ARSENAL WAMVALIA NJUGA KIUNGO WA REAL MADRID, YAPAMBANA NA UNITED KUMAPATA
Arsenal inataka kumsajili kiungo wa Korea Kusini na klabu ya Celtic, Ki Sung-yeung baada ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 kuwavutia wasaka vipaji wa klabu hiyo.
Matumaini ya Chelsea kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Hulk kutoka Porto yameanza kupungua baada ya Zenit St Petersburg kuweka dau la pauni Milioni 40, sambamba na kumtoa Bruno Alves, kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
Mazungumzo ya Arsenal kumsajili kwa mkopo Nuri Sahin kutoka Real Madrid yamefufuka, ingawa Liverpool, Tottenham na Manchester United kutajwa nazo kumuwania kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23.
Zenit St Petersburg ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Mbulgaria, Dimitar Berbatov, ambaye anataka kuondoka Old Trafford.
Chelsea inataka kumtumia Gael Kakuta kama chambo cha kumnasia beki Cesar Azpilicueta, mwenye umri wa miaka 22, kutoka Marseille.
Real Madrid imeongeza dau lake kwa ajili ya bLuka Modric hadi pauni Milioni 30m, lakini Tottenham inataka pauni Milioni 40.
Mchezaji anayewaniwa na Liverpool, Juan Manuel Vargas, mwenye umri wa miaka 28, amesema kwamba anafurahia kubaki nyumbani, licha ya kuhusishwa na mpango kuhamia Anfield.
Makamu wa rais wa Sao Paulo, Joao Paulo de Jesus Lopes amesema kwamba klabu yake imewasiliana na Paris Saint German juu ya kumsajili Lucas Moura, mwenye miaka 19, ambaye pia anatakiwaa ma Manchester United.
Roberto Martinez amemuambia Victor Moses kwamba atabaki Wigan, vinginevyo labda Chelsea iongeze lake hadi pauni Milioi 10.
Sunderland inajiandaa kukutana na Wolves kuomba kumnunu kwa dau la pauni Milioni 12, mshambuliaji Steven Fletcher, mwenye umri wa miaka 25.
Nigel Reo-Coker, mwenye umri wa miaka 28, anaifikiria ofa kutoka Serie A, baada ya kukataa ofa ya Fulham, kufuatia kuondoka Bolton.
Habari kamili: Daily Mirror
No comments:
Post a Comment