Friday, August 10, 2012

AFRICAN LYON YATANGAZA KOCHA MPYA.

Kocha mpya wa timu ya African Lyon inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Pablo Ignacio Velez kutoka Argentina wa kwanza kulia, akizungumzia nini atafanya akiwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao uliopangwa kuanza Septemba Mosi mwaka huu. Kocha huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo. Wengine katika picha ni Charles Otieno ambaye ni mkurugenzi wa ufundi na Biashara wa timu hiyo na Meneja Mkuu na Mmiliki wa timu hiyo, Rahim Kangezi. Picha na Mpiga picha wetu. 

No comments: