
Wanafunzi wa shule za msingi Vwawa wakiwa wanapiga vidumu huku wakielekea ofisi ya mkuu wa wilaya ni Baada ya walimu kugoma.

Wanafunzi wakiwa wanaelekea ofisi ya Mkuu wa wilaya.


Moja ya wanafunzi wa shule ya msingi Meta baada ya kuona walimu
hawajaingia darasani yeye alichukua jukumu la kuwafudnisha wenzake

Wanafuzi wapo makini kumsikiliza mwanafunzi mwenzao.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Makuburi,
wakijisomea baada ya walimu shuleni hapo kugoma kufundisha jana Julai
30, 2012. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ambaye hata hivyo alikataa kutaja
jina lake, alisema walimu walifika lakini hawakufanya kazi wakiunga
mkono agizo la rais wa chama cha walimu Gratian Mukoba, aliyewataka
walimu wote kushiriki mgomo usio na kikomo kuanzai leo Jumatatu.

Kiongozi wa wanafunzi walioandamana jana jijini Dar es Salaam,
Christofa Msifuni Msuya wa darasa la saba, shule ya msingi Bwawani,
akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye ofisi za Afisa Elimu wa Manispaa
ya Temeke jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 30, 2012.

Afisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam,
Juliana Mlay (Kushoto) akitafakari nini cha kuwaambia "Wageni" wake,
wanafunzi wa shule za msingi Kijichi na Bwawani za jijini walioandamana
umbali wa kilomita 10 hadi ofisini hapo wakilaani kutosoma jana,
kufuatia mgomo wa walimu ulioanza nchi nzima jana Julai 30, 2012.

Wanafunzi wa shule za msingi Bwawani na Kijichi, zajijini Dar es
Salaam, wakiamnadmana jana kupinga kile walichokiita kuvurfughwa kwa
haki ya mtoto ya kupata elimu, na hii ni kufuatia mgomno wa walimu
ulioanza jana nchi nzima. Wanafunzi hao waliandamana hadi urefu wa
kilomita 10 kutoka shuleni kwao hadi ofisi ya Afisa Elimu wa Manispaa ya
Temeke, ziliko shule hizo, jirani na uwanja wa taifa ili kufikisha
kilio chao.


Mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi muungano akiwa nje ya shule akichezea mchanga maana walimu wamegoma

Wanafunzi wa shule za Makuburi na Mabibo, wakiwa chini ya mwembe,
jana asubuhi Jumatatu Julai 30. Walimu wengi hawakuingia madarasani
kufundisha jana wakiitikia mwitoi kutoka chama cha walkimu nchini
kilichowataka kutofanya kazi jana Jumatatu na kuendelea hadi madai yao
kuhusu maslahi yatakaposhughulikiwa na serikali.

Wanafunzi
wa shule ya msingi Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani katika
Manispaa Singida.Picha Zote na Mdau Nathaniel Limu,Khalfan Hamis na
Wadau wa Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment