
Kufuatia
kuwepo kwa malalamiko ya vitendo vya Rushwa kuugubika ndani Muhimili
wa Bunge Tanzania na kusababisha kuvunjwa kwa kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini mwishoni mwa wiki iliyopita,
baadhi ya wabunge wametaka majina ya wenzao wanaojihusisha na Rushwa yawekwe wazi na wafukuzwe bungeni.
Akichangia
hoja mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Mbunge
wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari amesema licha ya kamati ya Nishati
na madini kutajwa moja kwa moja pia zipo kamati nyingine ambazo wabunge
wake wanatajwa kuhusika na vitendo vya kuomba rushwa.
Kwa
upande wao Mbunge wa Lindi Mjini Salum Khalfan na Mbunge wa Nkasi
Kaskazini Ally Keissy Mohamed wamelitaka bunge kuwafukuza bungeni
wabunge watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Baada
ya kutolewa kwa hoja hizo, Naibu Spika wa Bunge JobNdugai ameagiza
Kamati ya Uongozi wa Bunge kukutana na Spika Anne Makinda ili kulipatia
ufumbuzi suala hilo ambalo ni zito ndani ya chombo hicho cha kutunga
sheria.
Mbali na suala hilo ambalo limetikiza Bunge pia hii leo Waziri wa Afya na Uatawi wa Jamii Dk Hussein Mwinyi amewasilisha makadirio ya Bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 ambapo moja ya vipaumbele vyake ni kutatua tatizo la kuongezeka kwa vifo vya akinamama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua.
Kambi
rasmi ya Upinzani Bungeni nayo imepata fursa ya kuwasilisha Bajeti yake
Kivuli ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya ambayo imesomwa na
mbunge wa Viti Maalum Chadema, Conchester Lwamlaza.
No comments:
Post a Comment